THAMINI PROGRAM
Mpango wa Kuwezesha Wamiliki wa Ardhi Kuithamini na Kuiongezea Thamani Ardhi Yao
UTANGULIZI
Umiliki wa ardhi ni suala mtambuka linalohitaji taaluma mbalimbali ili kupata, kumiliki, na kuendeleza ardhi kwa maendeleo endelevu. Wamiliki wengi wa ardhi na mashamba wanakumbwa na changamoto kama:
- Kuiacha ardhi bila maendeleo, wakisubiri thamani ipande
- Hasara kwa kuzika fedha nyingi kwenye ardhi isiyoendelea
- Kupoteza ardhi kwa kuvamiwa au kuingia kwenye migogoro
- Kushindwa kuendeleza ardhi kwa vizazi na vizazi kutokana na changamoto za kifedha na usimamizi
Kwa kutambua changamoto hizi, BIG SALE AGENT CO. LTD imezindua THAMINI PROGRAM, mpango wa kusaidia wamiliki wa ardhi kuongeza thamani ya mashamba yao kwa njia endelevu kupitia huduma mbalimbali.
MIPANGO MIDOGO NDANI YA THAMINI PROGRAM
1. LEGAL SECURITY PLAN
Kuweka usalama wa umiliki wa ardhi kisheria na kupunguza migogoro. Inajumuisha huduma zifuatazo:
- Usajili wa Ardhi (Title Deed / Hati Miliki) - Ardhi inapaswa kusajiliwa kwa jina la mmiliki halali katika mamlaka ya ardhi.
- Ufufuaji wa Mipaka (Re-Demarcation) - Kufufua Mipaka na kuweka alama mpya za mawe kwa upimaji uliopoteza alama.
- Makubaliano ya Kisheria (Contracts & Leases) - Mikataba ya kisheria ikiwa ardhi inapangishwa au kuuzwa, lazima kuwe na mkataba wa kisheria.
- Ufuatiliaji wa Kesi na Migogoro (Legal Defense) - Kupatanishwa na Wakili au Mtaalamu wa ardhi anayeweza kusimamia kesi za aina hiyo.
- Uwekaji wa Alama za Tahadhari (Notice & Signage) - Mabango ya “No Trespassing” “Shamba Hili Haliuzwi”, “Shamba Hili linamgogoro” yanaweza kusaidia kuwazuia wavamizi wa ardhi.
Faida za Ulinzi wa Kisheria wa Ardhi:
- Unazuia kupokonywa ardhi kimabavu.
- Unaleta thamani kubwa kwa ardhi kwa sababu inakuwa na uhakika wa umiliki.
- Inafanya iwe rahisi kupata mikopo au wawekezaji.
- Inalinda ardhi kwa vizazi vijavyo.
- Inaepusha migogoro ya ardhi isiyoyalazima.
2. PHYSICAL SECURITY PLAN
Kuhakikisha ardhi inalindwa kimazingira na kimwili, kwa usafi, mipaka, na matumizi endelevu. Inajumuisha huduma zifuatazo:
- Uwekaji wa Mipaka (Demacation) - Uwekaji wa mipaka ya ardhi kwa kutumia nguzo imara za kudumu.
- Uhifadhi wa mazingira - Kupanda nyasi au miti kuzuia mmomonyoko wa ardhi.
- Ujenzi wa kibanda cha ulinzi na kuweka mlinzi wa shamba - Ulinzi dhidi ya wavamizi na watumiaji haramu wa ardhi.
Faida kwa Mmiliki wa Ardhi:
- Ulinzi dhidi ya wavamizi na watumiaji haramu wa ardhi.
- Mipaka ya kuaminika na ya kudumu.
- Ardhi kuwa katika hali nzuri kwa ajili ya uwekezaji au matumizi ya baadaye.
- Kujiandaa kwa hatua za kisheria au uwekezaji mkubwa.
3. DEVELOPMENT INVESTMENT PLAN
Kukuza na kuendeleza ardhi kupitia uwekezaji wa miundombinu na uzakishaji mali. Inajumuisha programu zifuatazo:
- Miundombinu na uwekezaji wa pamoja.
- Ushirikiano wa uzalishaji kati ya wamiliki na wawekezaji.
- Mikataba ya muda mrefu ya mauzo ya mazao (masoko).
Faida kwa Wamiliki:
- Ardhi kuanza kuzalisha mali au mapato.
- Kupata miundombinu bila mzigo mkubwa wa kifedha wa mtu mmoja.
- Kupata masoko ya uhakika na ushirikiano wa muda mrefu.
- Kuweka mazingira bora ya kupokea mikopo au kuvutia wawekezaji wengine.
JINSI YA KUJIUNGA NA MPANGO HUU:
✅ Fika moja kwa moja ofisini kwetu:
📍 Tegeta Kibo, Dar es Salaam – Jengo la Mjapani Complex ghorofa ya kwanza
📞 Piga simu au tuma ujumbe: 0743 223 880
🌐 Tembelea tovuti yetu: www.bigsaleagent.com
📲 Tufuatilie pia mitandaoni kwa jina: bigsale_co.ltd (Facebook, Instagram)